Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewatoa hofu Watanzania kwamba maswali yatakayoulizwa yote yanajibika na kuwasihi wayatafute maswali mapema na kuandaa majibu kabla makarani hawajapita kuwahesabu.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 23, 2022, jijini Dodoma mara baada ya yeye kuhesabiwa.
"Nataka niwatoe hofu wananchi kwamba zni kweli maswali ni mengi kidogo lakini hakuna swali gumu, maswali yote yanajibika, ombi langu kwa wananchi ni kuweka taarifa zao mapema," amesema Rais Samia.
Aidha Rais Samia ameongeza kuwa "Watu wetu wa takwimu, Makamisaa na timu zao walitoa maswali mapema, kwahiyo ni vyema kwa wale ambao hawajapata maswali wayatafute waanze kuyatafutia majibu mapema, ili karani wa sensa akisafika wanakwenda tu na majibu,".
No comments:
Post a Comment