Na: Mutaoba Arbogast,Bukoba
ASKOFU Dr Abdnego Nkamuhabwa keshomshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Magharibi,amewahimiza Wakristo na jamii kwa ujumla kuwa na moyo wa kusaidia watu wenye mahitaji maalum,wakiwemo watoto wadogo wanaolelewa katika Kituo cha malezi cha Ntoma,kilichoko kata ya Kanyangereko wilaya ya Bukoba.
Ameyasema hayo katika Harambee ya kuchangia kituo hicho mwisho mwa wiki,hafla iliyofanyika kituoni hapo ikiwajumuisha watu mbalimbali wenye mapenzi na watoto wadogo kuwasaidia katika makuzi na maendeleo ya awali kwao.
Askofu Keshomshara ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo amesema kuwa kila mmoja yupo kwa ajili ya mtu mwingine hivyo ukomavu wa mtu huonekana kwa jinsi anavyowajali wengine kama vile watoto;yatima na wajane.
Kituo hicho chenye umri wa miaka sabini,kikiwa chini ya kanisa hilo,tangu kuanzishwa kwake kimehudumia watoto wachanga 1290.
Kwa mujibu wa mkuu wa kituo hicho,Sr Penina Kaimukilwa,kituo hupokea watoto ambao mama zao hufariki wakati wa kujifungua,watoto ambao mama zao wamezikwa na akili,na watoto waliotelekezwa na mama zao,na hawafahamiki.
Amesema watoto wanaotunzwa hapo ni wale wenye umri kuanzia mwaka 0 hadi miaka miwili,na baada ya hapo hurudishwa kwenye familia zao,na endapo familia haina kabisa uwezo wa jumla mtoto,hupelekwa Kituo cha Betania Kemondo kinachohudumia watoto wa umri huo.
Sr Kaimukilwa amesema kwa sasa kituo hicho kunahudumia watoto 33,ingawa uwezo wao ni kulihudumia watoto 30,na ameiomba serikali kufuta kodi kwa misaada ambayo inatumwa na marafiki wa kituo hicho kutoka nje ya nchi kwani kufanya hivyo itakuwa imerahisisha watoto hao kuendelea kusaidiwa na Wasamaria wema, huku pia akiiomba kuwapatia ruzuku kama vile ilivyofanya miaka 28 iliyopita.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Uchangiaji huo,ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini,Dr Jasson Rweikiza amewashukuru wote waliojitokeza kuchangia akisema kumsaidia mwenye uhitaji ni kufanya kazi ya mungu.
Amesema kuwa Kamati ya maandalizi ililenga kukusanya michango ya shilingi milioni 27 badala yake imevuka lengo na kukusanya michango ya shilingi zaidi ya sh milioni 30 taslimu kwa ajili ya mahitaji ya watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Sherehe hiyo ya harambee ilitanguliwa na ibada ambayo imeongozwa na katibu mkuu wa Dayosisi ya Kasikazini Magharibi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Mchungaji Dr Elimeleck Kigembe.
Ni matumaini ya kituo hiki na vingine vya aina hii kufikiwa na matunda ya Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto kwa kuongea upatikanaji wa huduma za MMMAM,Ikiwa ni lishe bora,afya bora,maxingira salama?malezi yenye mwitikio na fursa za ujifunzaji wa awali .
No comments:
Post a Comment