Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk Albina Chuwa amesema adhabu anayostahili karani aliyefanya kosa la kupiga picha na kurekodi video wakati sensa ya watu na makazi ni faini ya Sh2 milioni, kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja.
Amesema ni kinyume cha sheria kwa karani yeyote kufanya hivyo anapochukua taarifa za wananchi na kwamba waliofanya hivyo, watachukuliwa hatua.
Akizungumza leo Agosti 28, katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya Sensa ya Watu na Makazi Mkoani Iringa, Dk Chuwa amesema taarifa zinazotolewa na wananchi ni siri.
Ameeleza kuwa tayari wameanza kuwachukulia hatua baadhi ya makarani waliofanya hivyo na kwamba, kulingana na sheria, adhabu ya kufanya hivyo ni kifungo cha miezi sita au faini ya Sh2 milioni au vyote kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment