DIWANI ATIMULIWA KWENYE BARAZA LA MADIWANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 26 August 2022

DIWANI ATIMULIWA KWENYE BARAZA LA MADIWANI



Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga amemfukuza Diwani wa Kata ya Kitangiri, Donald Ndaro katika kikao cha baraza la madiwani kinachofanyika katika ukumbi wa mikutano wa manispaa hiyo kwa madai ya utovu wa nidhamu.


Baada ya kufukuzwa diwani huyo alisimama kwa dakika zaidi ya tano akisubiri hoja za kumtetea kutoka kwa madiwani wenzake jambo ambalo liligonga mwamba baada ya mwanasheria wa ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Patrick Muhere kupigilia msumari kwamba Kanuni za Halmashauri za Uendeshaji wa Vikao hazimruhusu diwani huyo kuhudhuria kikao hicho.


Akizungumza na Mwananchi Digital katika mahojiano maalumu, Mulunga amesema uamuzi wa kumzuia diwani huyo kuhudhuria katika vikao viwili ulitolewa jana Alhamisi kutokana na utovu wa nidhamu.


Mulunga ameiambia Mwananchi Digital leo Ijumaa Agosti 26, 2022 kwamba diwani huyo (Ndaro) pamoja na kukatazwa kuzungumza bila ruhusa kutoka kwake ambaye ndiye mwenyekiti wa vikao vya baraza hilo alikaidi na kuendelea kuzungumza jambo lililosababisha usumbufu kwa wajumbe wa kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso