Mahakama ya Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe imemuhukumu miaka 30 jela Mwanaume aitwae Joseph Mwajombe (33) Mkazi wa kijiji cha Lulanzi, kwa kosa la kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 15.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo James Mhoni amesema Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 7, 2022 baada ya kutoka kumpakia Binti huyo kwenye pikipiki yake akitoka shuleni hadi eneo la jirani na nyumbani kwao alikomfanyia ukatili huo.
Hakimu amesema alipofika kwenye eneo hilo ambako kuna bwawa alimwambia Binti yake kuwa amewasiliana na Freemason ambao walibandika tangazo lao kwenye nguzo ya umeme ambao wamemuagiza afanye naye mapenzi ili apate utajiri hivyo akamuomba binti yake huyo amkubalie.
Hakimu amesema Mtoto huyo alikataa kufanya hivyo ndipo Baba huyo akampiga na kumuingilia kimwili kwa nguvu na baadaye kumrudisha binti huyo nyumbani kisha akaondoka kuelekea kusikojulikana na ilipofika usiku Binti alishindwa kuvumilia na kuanza kulia huku akimsimulia Mama yake kilichotokea ambapo Mama huyo akatoa taarifa upesi kwa Mtendaji wa kijiji aliyeongozana na Mgambo kumsaka na kumkamata Mtuhumiwa na kumpeleka Polisi ambako alikiri kutenda kosa hilo.
Chanzo:Millardayo
No comments:
Post a Comment