WANAKIJIJI BWEYUNGE MKOANI KAGERA WAPANIA KILIMO CHA MICHIKICHI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 16 August 2022

WANAKIJIJI BWEYUNGE MKOANI KAGERA WAPANIA KILIMO CHA MICHIKICHI



WANANCHI katika kijiji cha Bweyjnge,kilichoko kata ya Kanyigo wilayani Missenyi,wamekubaliana na azimio la Halmashauri ya kijiji kuhusu kutenga ardhi kwa ajili ya mashamba biashara(Block farming) kwa madhumuni ya kilimo cha michikichi.

Na Mutayoba Arbogast,Bukoba

Mwenyekiti wa kijiji hicho,Maxmiĺlian Bwikizo amesema tayari kijiji hicho kimetenga eneo lenye ukubwa wa hekta 194.


Amesema licha ya kutenga ardhi hiyo bado serikali ya kijiji inabaki na eneo jingine kubwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye.


 Pia kijiji kinachukua hatua ya kuwashawishi watu binafsi wenye maeneo yao ambayo yanafaa kwa kilimo cha michikichi,na yamekaa muda mrefu bila kuyaendeleza au yameendelezwa sehemu kidogo tu,nao wajiunge na mpango wa kilimo hiki,ambapo ardhi yaohiyo ina ukubwa wa hekta 104.


Endapo watu binafsi watakubaliana na mpango huu,basi jatarajio ni kuwa na jumla ya hekta 294 kwa ajili ya kilimo hicho.


Matarajio ya wananchi ni kuwa mradi huo wa mashamba biashara utawanufaisha kwa kuwepo miundo mbinu ya barabara inayozidi kujengwa,Hussain barabara ya Katoma-Kanyigo-Bukwali.


Afisa kilimo wa kata ya Kanyigo,Elieza Babu,aliyeshirikiana na Halmashauri ya kijiji katika mchakato wa kuibaini ardhi inayofaa kwa kilimo hicho,amesema tayari wamewasilisha mpango-mkakati na mapendekezo katika Halmashauri ya wilaya,idara ya kilimo na wanaendelea kusubiri  mrejesho.


Hata hivyo baadhi ya wananchi wameonesha wasiwadi juu ya soko wakasema wamewahi kulima alizeti lakini hukupokea mnunuzi na kuwa anaendeleaje kujibidiisha na kilimo cha vanilla ambao pia soko lake halitabiriki.


Rais Samia Suluhu Hassan,akiwa katika  ziara mkoani Kagera,Juni mwaka huu,aliuagiza uongozi wa mkoa kutanga hekta  70,000 hadi 100,000 kwa ajili ya kilimo cha alizeti na michikichi,ili kukabiliana na habari wa mafuta ya kula hapa nchini.


Wananchi wa kijiji Bweyunge wameitikia!

Aidha,katika hatua nyingine kijiji hicho kimekwishatenga pia kiasi cha ardhi kwa ajili ya mwekezaji wa utalii,ambaye anasubiriwa kukamilisha taratibu zote kwenye mamlaka husika ili kuanzisha shamba la wanyama,huku baadhi ya wananchi wakishauri shekau kubwa ya ardhi ya kijiji uendelee kibali wazi kwa matumizi ya baadaye ya vizazi vijavyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso