Watu watano wamefariki dunia akiwemo Mtoto mdogo katika ajali ya gari la Kampuni ya Tanzanite lenye namba za usajili T 916 DNU, ajali imetokea katika Kijiji cha Mbwasa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Stella Mukabiliwa amesema chanzo cha ajali hiyo iliyotokea Jana majira ya saa 9:30 Alasiri ni mwendokasi wa dereva uliosababisha tairi kupasuka ambapo baada ya ajali dereva alitoroka.
No comments:
Post a Comment