Wakati timu ya wataalamu kutoka nje ikitarajiwa kuanza uchunguzi kubaini ugonjwa usiojulikana Lindi, Wizara ya Afya imesema sampuli za vipimo vya maabara zilizochukuliwa kutoka kwa wagonjwa zimeonyesha siyo ugonjwa wa Ebola, Maburg wala Uviko-19.
Taarifa iliyotolewa Jana Ijumaa Julai 15, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza kwenye Kikao cha 22 cha Kisekta cha Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kilichofanyika Jijini Arusha.
“Kuna mlipuko wa ugonjwa usiojulikana Kusini mwa Tanzania (Lindi) na tayari timu ya watalaam wetu iko huko. Sampuli zimechukuliwa kutoka kwa wagonjwa na kuonyesha kuwa siyo ugonjwa wa Ebola, Maburg wala Uviko19,” amesema Waziri Ummy.
No comments:
Post a Comment