Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu ameipa tahadhari bodi mpya ya wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) kuwa biashara ya dawa ni miongoni mwa biashara hatari hivyo wanapaswa kuwa makini wakati wa utendaji wao huku akiipa siku 67 kuifumua bohari hiyo kiutendaji.
Amesema awali MSD ilifanya kazi zake vizuri na kuaminiwa na nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), hivyo ameagiza kurudishwa kwa mifumo ya tehama iliyosaidia kudhibiti mianya ya ubadhirifu ndani ya taasisi.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo Jumatatu Julai 25, 2022 wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti wake, Rosemary Slaa.
No comments:
Post a Comment