Mwenyekiti wa mtaa wa Luhende Msafiri Nadula
Taarifa hizo zimetolewa na mwenyekiti wa mtaa wa Luhende kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga Msafiri Nadula wakati akizungumza na Mwandishi wetu ambapo amesema tukio hilo limetokea Julai 18 Mwaka huu 2022 na kwamba watoto hao walikamatwa usiku wakiwa wamevaa nguo fupi.
Mwenyekiti Nadula amefafanua kuwa watoto hao baada ya kuwakamata walikiri na kwamba alichukua hatua za kuwafikisha kituo cha Polisi ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.
''Kuna wasamaria wema waliwaleta watoto wawili saa kumi usiku kwamba wamewakamata wakiwa wanadanga lakini mavazi yao waliyokuwa wamevaa ni kweli yalikuwa ya udangaji basi wakanikabidhi wao wakaondoka ikabidi niwahoji wale watoto wanaakili ni kweli nikawaambia sasa mlitoka hivi nyumbani na hizi nguo wakasema hapana tulivua hizo nguo tukaweka kwenye pagala wakanipeleka kwenye hilo pagala tukalikuta hilo furushi la hizo nguo zingine za nyumbani,"amesema.
"Nikawaambia kwa nini mnafanya namna hii mlikuwa wangapi wakasema tulikuwa watatu basi ikabidi niwapeleke polisi kwa kweli mavazi waliyokuwa wamevaa mpaka polisi walishangaa sana kwamba hiki kizazi cha wapi tena watoto wadogo miaka 11/12 wanafanya mambo ya namna hii ni kitu cha ajabu wakawahoji hoji polisi pale na kukiri walikuwa wanadanga'', amesema Mwenyekiti Nadula.
No comments:
Post a Comment