MTAALAM wa Sayansi ya elimu ya awali ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto(SECD) ambaye ni mmoja wa wawezeshaji kutoka Chuo Kikuu cha Aga Khan,Najma Rashid wa Mombasa, Kenya amewahimiza wazazi,walezi na wadau wote wa maendeleo ya watoto,kuhakikisha wanawaruhusu watoto wao kucheza,kwani ni kupitia michezo wakiwa wadogo, hujenga vipawa mbalimbali vitakavyowaongoza wakiwa watu wazima.
Bi Najma ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa mafunzo ya siku sita kwa wadau wa watoto 79,yaliyofanyjka lituo cha milutano cha St Gaspar,Dodoma,na wakati wa ziara ya kutembelea baadhi ya vituo vya malezi ya awalivinavyomilikiwa na jamii,ikiwa ni sehemu ya mafunzo hayo.
NA MUTAYOBA ARBOGAST,DODOMA
Katika vituo hivyo washiriki walijionea vitu mbalimbali wanavyochezea watoto wadogo,ambao husajiliwa kuanzia miaka mitatu hadi tano,kisha huenda katika madarasa ya awali ya shule za msingi.
"Wazazi na walezi wanatakiwa kufahamu kwamba makuzi,malezi na maendeleo ya awali ya mtoto yanaanzia miaka o hadi nane,pamoja na mambo mengine,fursa ya mtoto kucheza ni muhimu mno,na tunapowapeleka vituoni tusiwang'ang'anie kujua kusoma kuandika na kuhesabu bali stadi hizo watazifikia polepole kadri wanavyokua,tena kwa uzingativu zaidi,na kuwa wazazi wasihoji mbona watoto wanarudi kutoka shule wakiwa wamechafuka,wajue walikuwa wanacheza.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbande,Kata ya Sejeli,Wilaya ya Kongwa,Peter Chiyumbe,amesema kituo chao kinaendeshwa na wazazi kwa kuchangiamahindi kwa ajili ya uji na fedha kidogo ya kumlipa mpishi,huku malipo ya walezi wawili(wahudumu)wakisaidiwa na shirika la Blac.
Mkurugenzi wa maendeleo ya jamii,Chuo Kikuu cha Aga Khan Prof. Amina Abubakhar aliishukuru serikali kwa jinsi inavyojitoa katika kuhakikisha nasuala ya watoto yanapewa kipaumbele.
Mafunzo hayo yamefungwa mwishoni mw wiki na Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais,TAMISEMI,Ramadhani Kaitila aliyeahidi ushiriki na ushirikianocwa serikali katika kuhakikisha ustawi wa watoto unafikiwa,ambapo Chuo Kikuu cha Aga Khan kimewatunuku vyeti washiriki wa mafunzo.
Mafunzo hayo yameandaliwa na mashirika ya CiC,TECDEN na UTPC ikisa na lengo la kueneza elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya watoto.
No comments:
Post a Comment