WANAUME WATANO WAHUKUMIWA MIAKA 30 KILA MMOJA UTETEZI WAO WAKATALIWA -TABORA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 30 July 2022

WANAUME WATANO WAHUKUMIWA MIAKA 30 KILA MMOJA UTETEZI WAO WAKATALIWA -TABORA



Watu 5 wamehukumiwa kifungo cha miaka 150 jela baada ya kupatikana na hatia unyan’ganyi wa kutumia silaha katika eneo la Urasa kata ya Mambali wilaya ya Nzega mkoani Tabora.


Akitoa hukumu hiyo jana hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora Mhere Mwita alisema adhabu hiyo aliyoitoa iwe fundisho kwao na watu wengine wenye nia na tabia kama hizo katika jamii.


Waliopatikana na hati ni Media Kafula, Masanja Nkuba, Mashiri Buyinga, Wiliam Jeremia na Juma Sospeter ambapo mahakamani imeridhia kuwahukumu kifungo hicho cha miaka 30 jela  kila mmoja.


Alisema kwamba kutokana na kosa walilolifanya washitakiwa hao na ushahidi uliotolewa mbele ya mahakama hiyo usioacha shaka yoyote mbele ya mahakama hiyo tukufu.


Awali mawakili wa serikali kutoka ofisi ya mashtaka waliopo wilayani Nzega wakiongozwa na Jenifer Mandago waliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo Julai mosi mwaka 2021 watu hao watano Media Kafula, Masanja Nkuba, Mashiri Buyinga, Wiliam Jeremia na Juma Sospeter majira ya usiku wakiwa na silaha mbalimbali walivamia duka la Ufumba Kwirasa mkazi wa kitongoji cha urasa mambali na kumjeruhi kwa mapanga na kisha kumwibia zaidi ya shilingi laki saba pamoja na simu moja aina ya Tekno.


Mawakili hao wa serikali waliendelea kusema kwamba kutokana na kosa hilo la jinai namba 9/2021 wanaiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwao na kwa watu wengine wenye nia na tabia kama hizo.


Hata hivyo mahakama hiyo ilitoa nafasi ya utetezi kwao kabla haijawatia hatiani ambapo waliomba kupunguziwa adhabu kwani wanafamilia zinazowategemea.


Hakimu Mhere Mwita alitupilia mbali utetezi huo kwa kusema kwamba vijana wanatakiwa kutafuta fedha halali na sio kumwaga damu kwa watu waliojitafutia mali kwa jasho na wao kwenda kutumia nguvu kuzipora kwani hicho ni kitendo cha kikatili kwa jamii hivyo kifungo cha miaka 30 jela kwa kila mmoja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso