Mtaka ametoa agizo hilo leo Ijumaa Julai 22, 2022 wakati akizungumza kwenye mkutano na maafisa ardhi na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuhusu wimbi lililoibuka la wananchi kuvamia maeneo ya Serikali.
Mtaka amesema kumeibuka wimbi la wananchi hao kutwaa maeneo ya ujenzi wa miundombinu ya Kitaifa ikiwemo barabara ya mzunguko (ringroad) na uwanja wa Ndege wa Msalato kwa lengo la kudai fidia kinyume cha sheria.
"Kwa watakaotoa majina yao ndani ya siku saba wataruhusiwa kufanya hivyo bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria na kwa watakaokaidi agizo hili timu itafanya msako mkali kubaini wanaodanganya kuhusu zoezi hilo," amesema Mtaka
No comments:
Post a Comment