WAKULIMA MISENYI WAIOMBA SERIKALI KUCHUKUA HATUA VITENDO VYA UCHOMAJI MOTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 25 July 2022

WAKULIMA MISENYI WAIOMBA SERIKALI KUCHUKUA HATUA VITENDO VYA UCHOMAJI MOTO

WAKULIMA wilayani Missenyi Mkoani Kagera wameitaka serkari kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya uchomaji moto wiayani humo,vinavyosababisha moto huo wa nyoka kuunguza mashamba yao,yakiwamo ya miti na mazao ya shamba,na hivyo kuwasababishia hasara kubwa.


Na Mutayoba Arbogast,Bukoba


Moto huo ambao  huwashwa nyakati za kiangazi,miezi ya Juni hadi Agosti mwanzoni,huelezwa kuchomwa na wachungaji wa mifugo wakitafuta nyasi mpya,wawindaji,wakata mbao,warina asali,na hata wakulima wanaposafisha mashamba yao kwa moto.
Mmoja wa wakulima,miongpni mwa wengi waliopata hasara kubwa,ni Respicius John wa Kijiji cha Igayaza,Kata ya Nsunga,ambaye moto umeteketeza shamba lake la miti lenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 80.


"Yaani mtu unaweza kwa mtaji wako wote,jamaa wengine wapo wapo tu hawafanyi kazi,wanasubiri tu kuvutia hasara.Naiomba serikali ichukue hatua kali  kuonesha vitendo hivi vinavyoweza kuwakimbiza wawekezaji",amesema Johh.


Mkuu wa wilaya ya Missenyi,Kanali Willison Sakulo akiongea kwa simu na mwandishi wa habari hii,amesema anasikitishwa na viendo hivyo,na tayari wanachukua hatua pindi tu wahusika wanapofichuliwa,akitolea mfano wa mtu mmoja aliyekamatwa katika kata ya Minziro.


"Tatizo ni kwamba wananchi wenyewe mara nyingi hawako tayari kuwafichua wanaofanya vitendo hivyo ilhali wanawajua.Wanachi waache Tania ya "Kakitandugao" kwa maana ya mtu hataki jambo hilo la kuripoti lianzie kwake,na hali hiyo hutoa mwanya wa vitendo hivyo kuendelea",amesema,akiwasisitiza wananchi kutoa taarifa,na pia kamwe wasijiingize kwenye vitendo hivyo.


 Amesema ni hivi karibuni atakutana na watendaji wa kata kutoa mrejesho wa namna gani wanadhibiti vitendo hivyo,na kupanga mikakati mipya.


Licha ya kuharibu mashamba na mali nyingine za wananchi,mioto hiyo ni tishio kwa mali za serikali ikiwemo misitu na miundombinu ya umeme zikiwemo nguzo.


Pia moshi nzito hutanda barabarani na kutatiza magari na hata kusababisha ajali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso