LICHA ya mashindano ya mpira wa miguu kwa sasa kufanyika mara kwa mara katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, Wadau wa soka katika Wilaya hiyo wameishauri Halmashauri ya Manispaa kuboresha uwanja wa michezo kwa kupanda nyasi bandia kulingana na hadhi ya mji.
NA PAUL KAYANDA
Imeelezwa kuwa kwa vile michezo ni sera ya chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya uongozi wa Rais wa awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan na ametoa fursa ya kuboresha sekta hiyo kama kuwezesha nyasi bandia kuingia nchini pasipo na ushuru ni vyema viwanja vya michezo vikaboreshwa na kuleta ladha kwa watazamaji pamoja na wachezaji wenyewe.
Mwenyekiti msitaafu wa chama cha Mpira wa Miguu katika Mkoa wa Shinyanga(SHIREFA) Khamis Mgeja aliyasema hayo juzi alipokuwa akitoa zawadi kwa washindi baada ya mchuano timu ya vilab vya Kahama kwenye fainali ya ligi ya Mashujaa Cup iliyokuwa imeandaliwa na Redio Kahama FM ya Mjini Kahama.
“Ombi langu kwa manispaa yetu ya Kahama, sote tumeona Kahama ni wapenda burudani hasa katika Soka, pamoja na kazi kubwa inayofanywa na manispaa ya Kahama katika suala la uwanja bado.Vile vile kupitia ushirikiano mkubwa wabunge wa Majimbo matatu Kahama Mji, Ushetu na Msalala ombi langu waujenge uwanja huo,” alisema Mgeja.
Mgeja pia alikabidhi kiasi cha shilingi Milioni moja kwa timu ya Milango kumi ya Majengo na kiasi cha shilingi laki saba kwa Timu ya Ambasado ya Mjini Kahama.
No comments:
Post a Comment