BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara imevipiga 'stop' viwanja saba vilivyokuwa vinatumika kwenye ligi msimu uliopita hadi hapo vitakapofanyiwa marekebisho.
Viwanja vilivyosimamishwa hadi hapo vitakapofanyiwa marekebisho, la sivyo havitotumika kwa msimu ujao wa Ligi Kuu 2022/23 ni Mkwakwani Tanga, Ilulu Lindi, Ushirika Kilimanjaro, Mabatini Pwani, Sokoine Mbeya, Jamhuri Dodoma na Nyankumbu Girls, Geita.
Taarifa iliyotolewa jana na Idara wa Habari na Mawasiliano ya Bodi hiyo imesema kuwa wakati unasubiri taarifa ya ukaguzi wa viwanja unaofanywa na Kamati ya Leseni za Klabu iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imefanya tathmini ya viwanja vilivyotumika kwenye mechi za Ligi Kuu msimu uliomalizika na kubaini mapungufu kadhaa kwenye viwanja hivyo.
Taarifa hiyo imebainisha jumla mapungufu 10 ambayo yapo kwenye viwanja hivyo, kila uwanja ukiwa na mapungufu yake kadhaa, hivyo Bodi ya Ligi imezitaka klabu zinazotaraji kutumia viwanja hivyo kufanya jitihada za makusudi katika kuboresha maeneo yalioainishwa ili kukidhi matakwa ya kanuni na sheria zinazoongoza mpira wa miguu.
Baadhi ya mapungufu yalioainishwa kwenye viwanja hivyo ni eneo la kuchezea kutokuwa tambarare na kukosa nyasi za kutosha, pili ni ubovu katika uzio wa kutenganisha mashabiki na eneo la kuchezea, tatu vyumba vya kuvalia nguo za wachezaji na waamuzi kukosa sifa nne ambazo zimeainishwa pia.
No comments:
Post a Comment