Mkuu wa wilaya ya Misenyi Misenyi Mkoani Kagera Kanali Wilson Sakulo amemwagiza OCD wa wilaya hiyo kuhakikisha vinapotokea vitendo vya moto katika kata za wilaya hiyo viongozi wote kuanzia kwa Diwani, mtendaji wa kata mwenyekiti wa kijiji wakamatwe na kuwekwa ndani.
Na, Lydia Lugakila, Misenyi
Kanali Wilson Sakulo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mkutano wa baraza la madiwani robo ya nne , Aprili - Juni, 2022 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Kanali Sakulo ametoa maagizo hayo baada ya baadhi ya madiwani kutoka katoka katika baadhi ya kata zikiwemo za Bugorora, Bugandika kueleza kukithili kwa vitendo vya uchomaji moto sehemu za hifadhi kupitia taarifa za utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo katika kata zao.
" Moto wa mara kwa mara katika kata zenu inakera naagiza OCD kamata wote viongozi wa kata weka ndani sitarajii tena kusikia au kuona Moto ikiendelea katika kata wilaya yetu "alisema mkuu wa wilaya hiyo.
Ameongeza kuwa lazima hatua zichukuliwe ili ajulikane ni nani na nani wanajihusisha na vitendo ya uchomaji moto na kuwa kuna baadhi ya watu wanachoma moto bila kuchukuliwa hatua.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo ameagiza wananchi waliovamia msitu wa hifadhi wa Bushenya kuondoka mara moja huku watakao kaidi kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha amempongeza mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na diwani wa kata ya Kyaka Projestus Tegamaisho pamoja na madiwani wa Halmashauri hiyo kwa namna wanavyosimamia na kukusanya mapato ya Halmashauri hiyo.
Hata hivyo kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misenyi Projestus Tegamaisho amesema ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa mkuu wa wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment