Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu,kazi Vijana,ajira na watu wenye ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi amautaka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Shinyanga Mjini kuepuka kutumika vibaya kwa kufanya siasa za fitina zisizokuwa na tija.
Aidha amewaasa kuacha kuyumbishwa na kuyumbishwa na baadhi ya wanasiasa hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ndani ya chama hicho badala yake wazingatie misingi na haki.
Akizungumza wakati wa kuvunja baraza la Umoja wa Vijana wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,amesema wanahitaji kufanya siasa safi ambayo italenga kutatua changamoto zilizopo na kuleta maendeleo makubwa ndani ya chama na Taifa.
Katambi amewasihi Vijana kujisimamia wao wenyewe katika kufanya maamuzi kwa kupima jambo ambalo wameambiwa kufanya na siyo kukubali kutumika na kusababisha mpasuko ndani ya chama kitendo ambacho hawataweza kukivumilia na kwamba watachukuliwa hatua kali kwa kufuata taratibu za chama.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Majeshi akatumia fursa hiyo kuwataka Vijana kuwa makini,ikiwa ni pamoja na kuepuka kutumika kama vibaraka kwa baadhi ya watu na kuwasihi kufanya siasa safi na kufuata taratibu za chama.
No comments:
Post a Comment