Watu watatu wamefariki dunia kati 13 waliougua ugonjwa usiofahamika mkoani Lindi nchini Tanzania ambapo moja ya dalili zake ni kuvuja damu puani.
Taarifa hiyo inakuja siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzungumzia ugonjwa huo alipokuwa akifungua Mkutano mkuu wa 20 wa Shirikisho la mabaraza ya maaskofu wa Kanisa Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo Jumatano Julai 14, 2022 na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Alfello Sichalwe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Dk Sichalwe amesema ugonjwa huo umetokea katika Halmashauri ya Ruangwa mkoani Lindi ambapo kumekuwa na ugonjwa usio wa kawaida kutoka Kituo cha Afya Mbekenyera.
Soma zaidi: https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/video-ugonjwa-usiofahamika-waua-watatu-lindi-3878434
No comments:
Post a Comment