Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kiasi cha Shilingi trilioni 22.28 kati ya Julai 2021 hadi Juni 2022, sawa na ufanisi wa asilimia 99.22 ya lengo la makusanyo ya Shilingi trilioni 22.45.
Kiwango hicho ni sawa na ongezeko la Shilingi trilioni 4.13 ikilinganishwa na kiwango cha makusanyo ya Shilingi trilioni 18.15 kilichofikiwa kwa kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2020/21.
Ongezeko hilo ni sawa na ukuaji wa makusanyo kwa asilimia 22.77.
Kwa mujibu wa taarifa ya TRA iliyotolewa leo Julai 3, mwaka 2022 inaeleza katika robo ya nne ya 2021/22, makusanyo yalikuwa Shilingi trilioni 5.59 kati ya lengo la makusanyo ya Shilingi trilioni 5.3, sawa na ufanisi wa asilimia 105.47.
Aidha taarifa hiyo imesema Ufanisi huo wa kiutendaji ni matokeo ya kuendelea na matumizi ya mifumo ya kieletroniki katika usimamizi na ukusanyaji wa kodi, mazingira ya ufanyaji biashara nchini na mwenendo wa ulipaji kodi kwa hiyari.
No comments:
Post a Comment