Halmashauri ya Wilaya Same imetenga bajeti yenye mtazamo wa kijinsia kwa kuweka fedha za kuwezesha wasichana kupata taulo za kike wakati wa hedhi wakiwa shuleni.
Na Rodrick Mushi - Same
Hayo yamebainishwa Katika kikao kazi cha kupitia utekelezaji wa Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia kilichondaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na ONGAWA na wakuu wa Idara za Halmashauri na Mamlaka ya maji Vijijini (RUWASA), Halmashauri imefanikiwa kutekeleza shughuli mbalimbali za kijinsia kwa mwaka wa fedha 2021/2022 sambamba kuweka mikakati ya Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia.
Akizungumza wakati wa kikao hicho mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba, alisema kwamba, TGNP na ONGAWA walifanya utafiti shiriki wa Kijamii katika Halmashauri hiyo ambapo wananchi waliibua changamoto na kutoa mapendekezo kwa serikali namna ya kuzitaua ikiwepo kutenga bajeti. Ambapo hatua iliyofuata ilikuwa ni kuwajengea uwezo watendaji hao wa halmshauri na kuweka mpango kazi wa utekelezaji wa changamoto zilizoibuluwa.
Wilaya ya Same imefanikiwa kutumia zaidi ya milioni 11 kwa ajili ya kununua taulo za kike kwa shule za sekondari ambazo zimewanufaisha wasichana wapatao 9239, ambapo kwa shule za msingi wametumia kiasi cha tsh milioni 3,160, 000 kununua taulo za kike ambazo zimewanufaisha wasichana 117 wa shule za msingi.
Sambamba na hilo, bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya same na RUWASA Wilaya ya Same imewezesha upatikanaji wa maji kwenye shule za msingi, sekondari na zahanati sambamba na ujenzi wa matundu ya vyoo yenye vyumba maalum vya kujisitiri wakati wa hedhi.
“ Pamoja na mafunzo tuliyoyatoa kwa hawa watendaji wa serikali, pia tumezingatia kwamba wakati wa utafiti wa kiraghibishi kuna mapendekezo yalitolewa, ndio hayo pia tunaangalia kwenye vitabu vya bajeti zao kama wametenga fedha na utekelezaji wake.” Alisema Temba
Aidha ameongeza kwamba, kwa kipindi cha miaka miwili, halmashauri ya wilaya ya same imefanya vizuri kwenye eneo la Bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa sababu wameweza kutenga fedha kwaajili kutoa taulo za kike mashuleni, ujenzi wa matundu ya vyoo yenye vyumba maalum vya kujisitiri wasichana wakiwa kwenye hedhi, sambamba na kusongeza maji katika shule za zahanati.
Mbali na ununuzi wa taulo za kike Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Same Benedict Michael anasema walijikita kutekeleza bajeti yenye mtazamo wa kijinsia kupunguza changamoto zinazomkabili wanafunzi wa kike ikiwemo ujenzi wa mabweni ili kuondokana na changamoto ya mimba za utotoni zinazosababishwa na wanafunzi kurubuniwa kutokana na kutembea umbali mrefu.
Kwa upande wake Afisa elimu idara ya sekondari, Wilayani humo Adinani Mwenda alisema licha ya jitahada ambayo imekuwa ikifanywa ya kutenga majeti kwa mtazamo wa kijisnia lakini bado kuna changamoto ya baadhi ya miradi ambayo inatekelezwa kutokamilika kwa wakati kutokana na fedha ambazo zimekuwa zikiletwa na serikali kutokutosha kukamilisha miradi hivyo kuiomba serikali kuhakiki (kureview) bajeti ya miundombinu ya mabweni ili fedha zinazoletwa kuweza kukamilisha ujenzi wake haki kukamilika.
Chanzo:Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment