Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Dkt. John Nkengasong ambaye ni Mratibu wa Serikali ya Marekani katika kupambana na UKIMWI duaniani na msimamizi wa mfuko wa Rais wa Marekani wa kudhibiti UKIMWI (PEPFAR).
Prof. Makubi na Mhe. Dkt. Nkengasong wamekutana wakati wa Kongamano la UKIMWI duniani linalofanyika mjini Montreal, Canada ambako walijadiliana kuhusu jinsi ya kuboresha ushirikiano kati ya PEPFAR na Serikali ya Tanzania katika kudhibiti UKIMWI.
Prof. Makubi amempongeza Dkt. Nkengasong kwa uteuzi wake wa kihistoria na kumuomba kushirikiana zaidi na PEPFAR katika kuwekeza Tanzania kwenye viwanda vya bidhaa za huduma za afya.
Vile vile umuhimu wa kuboresha utoaji wa huduma za afya na kutumia watoa huduma za afya ngazi ya jamii kwa kuwa kuna upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali za afya.
Aidha, Prof. Makubi aliongelea umuhimu wa kutambua ongezeko la kasi la magonjwa yasiyoambukizwa kama Kisukari, Shinikizo la damu na unene uliopitiliza.
Prof Makubi aliishukuru PEPFAR kwa kuijuimisha Tanzania kuwa kati ya nchi chache zitakazo tekeleza mkakati maalumu wa kutokomeza UKIMWI kwa Watoto. Mwisho Prof. Makubi alimkaribisha Mhe. Dkt. Nkengasong kutembelea Tanzania.
Balozi Nkengasong alisisitiza umuhimu wa nchi kujipanga na kuhakikisha uendelevu wa mwitikio wa mapambano dhidi ya UKIMWI. Katika kuendeleza ushirikiano kati ya serikali hizi mbili Balozi Nkengasong ameahidi kuja kutembelea Tanzania
No comments:
Post a Comment