MWENGE WA UHURU WAENDELEA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 27 July 2022

MWENGE WA UHURU WAENDELEA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA SHINYANGA




KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, amezindua na kuweka mawe ya Msingi kwenye Miradi ya Maendeleo Manispaa ya Shinyanga, na kushiriki ujenzi wa Jengo la Utawala Manispaa ya Shinyanga.


Na Marco Maduhu-Malunde 1 blog


Mwenge huo wa Uhuru umekimbizwa leo Julai 27,2022 katika Manispaa ya Shinyanga, ukitokea halmashauri ya Shinyanga, ambao umepitia Miradi Mitano ya Maendeleo na yote imekubaliwa.


Akizungumza wakati akikagua Miradi hiyo ya maendeleo kwa nyakati tofauti, Geraruma amesema Miradi yote ni mizuri na ameridhia kuweka Mawe ya Msingi pamoja na kuizindua.


"Miradi yote ya maendeleo ambayo nimeipitia ni mizuri na ile ambayo nimetoa maelekezo ifanyiwe marekebisho na kuendelea kutoa huduma bora kuwa wananchi," amesema Geraruma.


Katika hatua nyingine, ametoa wito kwa wananchi wa Shinyanga siku ya Kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu, wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa.


Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye ulemavu, amepongeza usimamizi mzuri wa Miradi hiyo ya maendeleo na kutumia fedha vizuri ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Rajab Masanche, awali akipokea Mwenge huo wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Nice Munissy amesema Mwenge huo utazindua Miradi ya maendeleo Miwili ambayo ni Ujenzi wa Zahanati ya Shushu na Mradi wa Maji Bugwandege.


Amesema Mwenge huo pia umeweka Mawe ya Msingi katika Kiwanda cha Bia cha Gaki Investment, ujenzi vyumba vya Madarasa Sita na Ofisi mbili za walimu katika Shule ya Msingi Ugweto. Pia Mwenge huo ulipita kwenye viwanja vya Mazingira Center.


Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu (2022) inasema "Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo, Shiriki kuhesabiwa kwa Maendeleo ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso