MWANAUME AUA MKE WAKE KISA ELFU 10-MTWARA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 26 July 2022

MWANAUME AUA MKE WAKE KISA ELFU 10-MTWARA




Maria Sakware, mkazi wa mkoa wa Manyara, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa fimbo na mume wake aitwae Petro Fabiano, na kumsababishia majeraha katika mguu wa kushoto na kumvunja mkono wa kushoto kwa kumtuhumu kuwa amechukua elfu 10.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara ACP Benjamin Kuzaga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


"Timu ya makachero baada ya kufuatilia kiini cha tukio hili ilibainika kuwa huyu mume alikuwa akimpiga kwavmadai kwamba haoni shilingi elfu kumi kwahiyo akiwa anamtuhumu kwamba amemchukulia, ndiyo kilichokuwa chanzo cha kipigo hadi kupelekea kufa," amesema kamanda Kuzaga


Aidha Kamanda Kuzaga, amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wanapowabaini wahalifu na siyo kushirikiana nao.

chanzo:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso