Marwa Nyamuhanga (33) mkazi wa Nyabisare Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, mkoani Mara amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba.
Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma, Hakimu Mkazi Mwandamizi Stanley Mwakihaba, Mwendeshesha mashtaka mwanadamizi wa serikali Monica Hokororo, amesema mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi ya jinai no 7 ya mwaka 2022 ikiwa ni kinyume na kifungu cha Sheria no.130 (1),2 (e) na kifungu cha 131 (1) cha kanuni ya adhabu kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Hokororo amesema mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Desemba7, 2021, katika eneo la Nyabisare ambapo mtuhumiwa alimwita mtoto huyo na kumpatia shilingi 500 na kumtuma akamnunulie maandazi na kisha kumwingiza katika pagala la nyumba na kuanza kumtendea unyama huo ambapo alitimiza adhima yake ya ubakaji.
Mwendesha mashitaka ameendelea kuambia Mahakama hiyo kuwa mshtakiwa huyo wakati akiendelea kumbaka mtoto huyo mtoto alikuwa akipiga kelele za kuomba msaada ndipo dada wa muathiriwa na mama yake walifika eneo la tukio na kumkuta kijana huyo Marwa akiwa anatenda tendo hilo la ubakaji.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi Stanley Mwakihaba, amesema Mahakama hiyo imethibitisha pasi kuacha shaka ya aina yoyote kwa mshtakiwa huyo kuwa ametenda kosa hilo la ubakaji.
CHANZO:EATV
No comments:
Post a Comment