Mwalimu wa shule ya msingi Kyawazaru Idrisa Athumani (29) mkazi wa wilayani Butiama mkoani Mara, amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za ulawiti wa wanafunzi wanne katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma na kusomewa mashtaka manne kwa mahakimu wanne wa Mahakama hiyo.
Akisoma mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali Tawabu Issa, amesema mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka manne ya ulawiti ambapo shtaka la kwanza alisomewa kwa Hakimu Mkazi Mwanadamizi Stanley Mwakihaba, ambapo mshtakiwa huyo ametenda makosa hayo kwa nyakati tofauti ikiwa ni kinyume na kifungu cha Sheria No. 154 kifungu cha kwanza (a)cha kanuni ya adhabu sura ya 16 ya mwaka 2019.
Aidha Mwendesha mashtaka Yahya amesema mtuhumiwa huyo ametenda tena kosa la ulawiti na shtaka hilo lipo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma Hakimu Timoth Swai.
Mashtaka mengine ya ulawiti yapo kwa Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Hakimu Erick Marley, pamoja Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma Eugenia Rejwahuka na upelelezi wa mashauri hayo umekamilika ambapo mtuhumiwa huyo baada ya kusomewa mashtaka yake mbele ya mahakimu hao mtuhumiwa huyo alikana kutenda makosa hayo.
Aidha Hakimu Mwakihaba amesema kuwa dhamana ya mtuhumiwa iko wazi iwapo wadhamini hao wakikidhi vigezo wanaweza kumdhamini kwa mujibu wa sheria.
Kesi zote zimeahirishwa mpaka Agosti 4 mwaka huu ,mtuhumiwa amekosa wadhamini na amerudishwa rumande.
chanzo:EATV
No comments:
Post a Comment