MTUMISHI ALIESEMA HATA AKIFUKUZWA KAZI AKAMATWA NA KUWEKWA NDANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 6 July 2022

MTUMISHI ALIESEMA HATA AKIFUKUZWA KAZI AKAMATWA NA KUWEKWA NDANI



Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel ameagiza kuondolewa madarakani kwa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa wizara hiyo, Paul Koroso kutokana na mgogoro ulioibuka katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh2.9 bilioni.


Dk Mollel pia ameagiza Koroso aswekwe mahabusu akidai amemtolea majibu na lugha ya kijeuri kuwa “hajali lolote hata akifukuzwa kazi”.


Dk Mollel ametoa maagizo hayo Julai 5 akiwa mjini Nansio Ukerewe alipofika kutatua mgogoro uliobuka kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi hospitali ya Rufaa ya mkoa katika kisiwa hicho ndani ya Ziwa Victoria.


"Kutokana na changamoto zilizojitokeza kwenye mradi huu, Koroso utakoma kuwa mkuu wa Idara ya Ujenzi Wizara ya Afya. Katibu mkuu atamteua mkuu mpya wa idara ambaye atakuja kusimamia mradi wa Ukerewe," alitangaza Dk Mollel.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso