MTAMBO WA KISASA WA KUNYONYA TOPE KINYESI KWENYE MAKAZI YA WATU WAZINDULIWA SHINYANGA MJINI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 16 July 2022

MTAMBO WA KISASA WA KUNYONYA TOPE KINYESI KWENYE MAKAZI YA WATU WAZINDULIWA SHINYANGA MJINI


Uzinduzi wa Mtambo wa kisasa wa kunyonya tope kinyesi kwenye vyoo ukizunduliwa katika choo cha Ngokolo Mitumbani Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA


MANISPAA ya Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) wamezindua Mtambo kwa kisasa (PITVAQ) wa kunyonya tope kinyesi (Majitaka) kwenye vyoo vya Makazi ya watu, maeneo ya Masoko na Ofisi mbalimbali.


Mtambo huo umezinduliwa leo Julai 15, 2022 katika Choo cha Ngokolo Mitumbani Manispaa ya Shinyanga na kufanya mafunzo ya vitendo kwa watakao utumia.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtambo huo Afisa Afya Manispaa ya Shinyanga Sanya Anthony, amesema Mtambo huo wa kisasa wa kunyonya tope kinyesi kwenye vyoo umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) kupitia mradi wao wa usafi wa Mazingira.


Amesema Mtambo huo wenyewe unanyonya kila kitu ndani ya Choo na kubaki cheupe hakuna hata tope, tofauti na magari ya majitaka ambayo yenyewe yananyonya maji tu, na hakuna uchafuzi wa mazingira wala utoaji wa harufu kali wakati unyonyaji tope hilo.


“Tunalishukuru Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) kwa kutufadhili Mtambo huu wa kisasa ambao utatumika kunyonya tope kinyesi kwenye vyoo, na kisha kuupeleka kwenye Mtambo mkubwa wa kuchakata na kutibu tope kinyesi uliopo Nhelegani, na kuuweka mji wa Shinyanga katika hali ya usafi wa Mazingira,”amesema Anthony.


“Mtambo huu utasaidia pia watu kuacha kuingia ndani ya mashimo ya vyoo kwa ajili ya kusomba tope kinyesi na kuhatarisha afya zao, na utakabidhiwa kwa kikundi kinaitwa watu kazi, ambao ndiyo watakuwa wakifanya kazi hii ya kusomba tope kinyesi kwenye vyoo,”ameongeza.


Nao baadhi ya wananchi ambao wameshuhudia Mtambo huo wa kisasa wa kunyonya tope kinyesi kwenye vyoo, wameipongeza Serikali na wadau wa maendeleo kwa kujali afya za wananchi, na kuendelea kuimarisha masuala ya usafi wa mazingira.


Uzinduzi wa Mtambo wa kisasa wa kunyonya tope kinyesi kwenye vyoo ukizunduliwa katika choo cha Ngokolo Mitumbani Manispaa ya Shinyanga.

Uzinduzi wa Mtambo wa kisasa wa kunyonya tope kinyesi kwenye vyoo ukizunduliwa katika choo cha Ngokolo Mitumbani Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Tope kinyesi likipelekwa katika Mtambo mkubwa wa kuchakata na kutibu tope hilo maeneo ya Nhelegani Manispaa ya Shinyanga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso