Madiwani wa Jiji la Arusha wamemshukia Mkuu wa Mkoa huo, John Mongela wakidai amewadhalilisha kwa kuwaita wapika majungu, wafitini na wanakwamisha maendeleo.
Wiki iliyopita, Mongela akiwa kwenye kikao na madiwani wa jiji la Arusha na watendaji wa jiji hilo kujadili ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), aliwatuhumu madiwani kuwa na majungu, kufitiniana na hivyo kukwamisha maendeleo ya jiji, ikiwemo ujenzi wa kituo kipya cha mabasi.
Jana akizungumza kwa niaba ya madiwani wenzake, Diwani wa Ngarenaro, Isaya Doita alisema wamesikitishwa na tuhuma za Mongella alizotoa hadharani juu yao, ambazo zimewadhalilisha na kulikuwa na fursa ya kuzungumza kupitia vikao vya chama kwani wao ni madiwani wa CCM.
“Tumeomba kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, tujadiliane atueleze matatizo yetu ili kama ni kweli tujirekebishe, lakini ninachojua mimi hakuna diwani ambaye ni kikwazo cha maendeleo,” alisema.
No comments:
Post a Comment