Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shule ya Msingi ya King David, David Chibunu anashikiliwa na vyombo vya usalama kufuatia ajali ya basi iliyosababisha vifo vya watu 13 wakiwamo wanafunzi 11.
Ajali hiyo ilitokea jana Jumanne eneo la Mjimwema, Kata ya Mikindani, Mtwara Mjini na kusababisha vifo vya watu 13, kati yao ni wanafunzi 11 wa Shule ya Msingi ya King David na watu wazima wawili.
Akizungumza leo Jumatano Julai 27, 2022, mmiliki wa Shule hiyo, Alex Chibunu amesema David ambaye pia ni meneja wa shule hiyo anashikiliwa na vyombo hivyo vya usalama.
No comments:
Post a Comment