Akizungumza na Nipashe kwenye banda la chuo hicho, mwanafunzi wa Sayansi ya Uzamili wa chuo hicho, Nelson Kissanga, alisema wamegundua mkojo wa sungura unaharufu kali na sio rafiki kwa wadudu hususani wale waharibifu katika mboga zenye jamii ya maua na matunda.
Kissanga alisema kugundua mfumo huo kutasaidia mimea ya wakulima kuwa salama na pia wameunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa Tanzania ni mahali sahihi pa biashara na uwekezaji.
"Tumekuja na ubunifu huu ambao utasaidia wakulima kutopata hasara pindi wadudu watakapoingia katika bustani na mashamba yao kuharibu mboga na matunda," alisema Kissanga.
"Wadudu wengi huvutiwa sana na mvuto wa mboga na matunda kwa sababu hufuata harufu nzuri hasa yanapochanua, ni waharibifu katika mboga na hususani jamii ya maua pamoja na matunda." Alisema mkojo huo wa sungura ni mbadala wa utumiaji wa kupuliza dawa katika mboga na matunda. "
Mkojo huo wa sungura ni fursa kwa watu wengi kwa sababu unapowafuga na kupata mkojo wao, mfugaji anapaswa kujenga banda la juu ili wanapokojoa kunakuwa na kinga," alisema Kissanga.
No comments:
Post a Comment