Mahakama Kuu ya Tanzania imepanga kusikiliza kesi ya waliokuwa wanachama na Chadema, Halima Mdee na wenzake 18 wanaopinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho, Agosti 26,2022.
Tarehe hiyo imepangwa na Jaji Cyprian Mkeha, wakti kesi hiyo ilipoitwa leo Ijumaa Julai 29, 2022 kwa ajili maelekezo muhimu.
Vile vile mahakama imewataka Mdee na wenzake saba kufika mahakamani siku hiyo ya usikilizwaji kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano na mawakili wa Chadema.
Jaji Mkeha ametoa amri hiyo dhidi ya kina Mdee kufuatia ombi lililotolewa na kiongozi wa jopo la mawakili wa Chadema, Peter Kibatala kuomba waitwe ili waweze kuwafanyia mahojiano.
Mbali na Mdee wengine walioitwa ni Nusrati Hanje, Ester Matiko, Ester Bulaya, Jesca Kishoa, Grace Tendega, Hawa Mwaifunga na Cecila Pareso.
Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama.
No comments:
Post a Comment