Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Menrad Sindano akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma amesema kuwa tukio hilo lililotokea juzi majira ya saa mbili usiku kijijini hapo ambapo majambazi waliouawa wanadaiwa kuwa ni raia wa Burundi.
Sindano alisema kuwa katika tukio hilo majambazi hao wakiwa watatu wakitumia budnuki aina ya AKA 47 walipora vitu mbalimbali ikiwemo vitenge, simu na pesa taslimu katika maduka matatu likiwemo dula la dawa, vitenge na kibanda cha M-pesa.
“Baada ya tukio hilo wananchi waliripoti tukio hilo kituo cha polisi Gwanumpu wakiomba msaada baada ya kuwazingira majambazi hao wakiwarushia mawe ndipo askari polisi na jeshi kutoka kikosi cha mpakani cha Bukirilo walifika eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi ambapo majambazi wawili walijeruhiwa vibaya na mmoja alifanikiwa kukimbia,”Alisema Kamanda Sindano.
Alisema kuwa baada ya majibizano ya risasi na majambazi hayo kujeruhiwa walifariki njiani wakipelekwa hospitali ya wilaya Kakonko ambapo msako unaendelea kumtafuta jambazi mmoja aliyekimbia.
Katika tukio hilo Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma alisema kuwa walifanikiwa kukamata bunduki moja aina ya AKA 47 ikiwa na magazine mbili na risasi 15 sambamba na maganda matatu ya risasi, simu tisa walizokuwa wamepora na fedha taslimu shilingi 82,000/
Kamanda Sindano alisema kuwa katik upekuzi huo marehemu hao walikutwa na vitambulisho viwili kwenye nguo zao na kutaja majina kwenye vitambulisho hivyo kuwa ni Harelimana Ananias (30) na Nimpangalitse Jean (36) wakazi wa mkoa Ruyigi nchini Burundi.
chanzo:Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment