Mahakama ya wilaya mkoani Arusha, imemhukumu kifungo cha maisha jela, Fadhili Kivuyo (29) mkazi wa Olturumet wilayani Arumeru baada ya kutenda makosa mawili ya kumbaka na kumlawiti mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka sita,ambaye amelazimika kujisitiri kwa Pambas muda wote .
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Gwantwa Mwankuga, alisema kuwa mahakama hiyo ilimtia hatiani mshtakiwa kwa kutenda makosa yote mawili kwa ushahidi usio acha shaka uliotolewa na upande wa jamhuri.
Kesi hiyo namba 31/2021 mshtakiwa alitenda makosa mawili ambapo kosa la kwanza la ubakaji mahakama ilimhukumu kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia.
Alisema kosa la pili ni kulawiti ambapo mahakama hiyo ilimkuta na hatia na kumhukumu kifungo cha maisha jela,ambapo katika adhabu hizo mshtakiwa atatumikia adhabu moja ya kifungo cha maisha jela
Awali mwendesha mashtaka wa kesi hiyo,Lilian Mmasi aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia Kama hiyo, ukizingatia kwamba umri wa mtoto huyo ni mdogo na ameharibiwa kisaikolojia.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mwankuga alisema kuwa mnamo,Mei 19,2021 majira ya saa 2 usiku mshtakiwa, Fadhili Kivuyo maarufu kwa jina la Toll,akiwa mlinzi wa nyumba binafsi eneo hilo,alimrubuni mwanafunzi huyo(jina limehifadhiwa) akiwa ametumwa dukani na mama yake na kumvutia katika eneo alilokuwa akilinda na kumfanyia vitendo vya ukatili kwa kumbaka na kumlawiti.
Baada ya hukumu hiyo mmoja ya watetezi wa haki za watoto mkoani Arusha,Mama Hindu Mwego ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la Center for women and children development (CWCD)aliishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki ,akidai hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa watu wote wenye tabia Kama hiyo.
Aidha mama Hindu aliwatahadhalisha wenye tabia kama hiyo wakidhani mahakama zipo likizo kuwa ,watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria na kuitaka jamii kuhakikisha inaungana kukemea matukio ya aina hiyo ambayo huachwa yamalizike kinyumbani au wahusika kushindwa kutoa ushahidi mahakamani.
Naye afisa ustawi wa jamii katika halmashauri ya Arusha,Josina Mlaki pamoja na kuishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki alisema kuwa bado changamoto ya ukatili kwa watoto ni kubwa.
Alisema katika halmashauri hiyo matukio ya ukatili ni mengi, hivyo aliiasa jamii kukomesha matukio hayo kwa kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahakifu na kutoa ushahidi mahakamani.
Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto aliyefanyiwa ukatili,Ester Efrahim alisema kuwa siku ya tukio alimtuma mtoto wake dukani lakini alikaa kwa muda Bila kumwona na ndioo alipoamua kutoa taarifa kwa balozi ambapo majira ya saa tatu usiku walifanikiwa kumkuta mtoto barabarani akilia kwa uchungu na kutetemeka .
Alisema kuwa baada ya kumhoji ,mtoto wake alieleza kuwa alichukuliwa na kuingizwa katika chumba cha mlinzi huyo kwa zaidi ya saa moja akimbaka na kumlawiti ndipo walipoamua kumpeleka kutibiwa hospitalini na kugundulika kuwa ameharibika vibaya sehemu zake za siri ambapo hadi hivi Sasa anatumia Pempazi kujistili kutokana na haja kubwa kutoka lenyewe muda wote.
Chanzo:a24habari
No comments:
Post a Comment