WAKRISTO Wakatoliki na jamii kwa ujumla,wamehimizwa kuwajali watoto wadogo nyakati za sherehe na matukio mengine kwa kuwaundia Kamati ya kuwahudumia,badala ya kuwa na Kamati ya kuwafukuza watoto.
Hayo yamesemwa na Padri Patrick Tibangayuka,wakati wa mahubiri Dominika ya 16 ya mwaka C,katika kigango cha Bugombe,Parokia Katoliki ya Kanyigo,Jimbo la Bukoba.
Na Mutayoba Arbogast,Bukoba
Padri Tibangayuka ambaye ni mzaliwa wa Parokia ya Kanyigo,akifanya utume katika Seminari kuu ya Nazareth-Mwendakulima,Jimbo la Kahama,ambaye yuko kwenye shughuli jimbo la nyumbani.
Katika Injili Lk 10:38-19....Bwana akajibu "Martha,Martha,unasumbuka na ufadhaika kwa ajili ya vitu vingi,lakini kinatakiwa kitu kimoja tu,na Mariam amechagua fungus lililo jema,ambalo halitaondolewa"
Akinasibisha na injiii hiyo amesema ni jambo la kusikitisha sana siku hizi nyakati za sherehe na matuki mengine,kuwaona watoto wakibaguliwa wakati wa chakula,bila kuwekewa mtu maalum mwenye upend na kujali,wala hata hawatengewi nafasi yaani banda lao,na hivyo hula kwa bahati naibu.
"Nakumbuka huko nyuma sherehe ya kuoza au kuozeshaa ilikuwa shughuli ya kijiji chote,na mngegombana na mtu ambaye huenda kwake kuchukua Mungu wa ndizi aliokuandalia,kulikuwa na upendo mkuu,watoto tulikula,tulikunywa na kufurahi."
Amesema,sasa watoto hawathaminiwi tena jinsi inavyostahili,badala take kamati mbalimbali zinaundwa kuwahudumia watu wazima,hakuna kamati ya watoto na mbaya zaidi inaundwa kamati ya kuwafukuza au kuwadhibiti watoto.
"Utakuwa mtu amechangia gharama za bia nane,na anataka 'azifute' peke yake, kumbe angepewa bia mbili,nyingine zikagharamia soda kwa watoto.
Naomba niwaachie hili,lila mnapoandaa sherehe au tukio,undeniably Kamati ya kuwahudumia watoto,hao ni malaika wadogo,na kupitia furaha yao kuna kujaliwa kwingi",amesema Padri Tibangayuka.
Programu Jumuishi ya Taifa ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto(PJ-MMMAM)inamhiza kila mdau wa maendeleo ya jamii kuwapa umuhimu watoto ili wafikie kiwango kinachokidhi makuzitimilifu,kimwili, kiakili,kiroho,kimaadili na kijamii.
No comments:
Post a Comment