Ameagiza waganga wakuu kwenye mikoa kutopuuza dalili za ugonjwa wowote unaolipuka kwenye jamii na badala yake wafufue timu za ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko.
Julai 12, akihutubia Mkutano wa 20 wa Shirikisho la Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (Amecea) Rais Samia Suluhu Hassan alitoa taarifa ya ugonjwa huo mpya kuingia mkoani Lindi ambapo baadhi ya watu waliripotiwa kutokwa na damu puani na kuanguka, hadi sasa watu 20 ndio wameripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo na watatu kufariki.
Akizungumza Dar es Salaam leo Julai 29 Waziri Ummy alisema hadi sasa hakuna mgonjwa aliyelazwa na kwamba wananchi waondoe wasiwasi kwani ugonjwa huo unatibika kwa antibiotics.
"Timu ya wataalamu imefuatilia na kubaini watu waliochangamana na wagonjwa hawakuambukizwa ugonjwa huo, hii inadhihirisha ni mara chache ugonjwa huu kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine," amesema.
Ummy amesema ugonjwa huo sio tishio tena hapa nchini kwa kuwa matibabu yake yapo hivyo wizara haitokuwa ikitoa ikitoa taarifa za ugonjwa huo badala ameagiza watoa huduma za afya kote nchini kutoa taarifa za ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment