DK MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI ITAKAKAYOHUDUMIA ROMBO, KENYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 18 July 2022

DK MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI ITAKAKAYOHUDUMIA ROMBO, KENYA



Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango ameweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, ambayo kukamilika kwake kunatajwa kutaondoa adha ya kupata matibabu waliyokuwa wanaipata wananchi wa ukanda wa chini wa wilaya hiyo na baadhi ya vijiji vya nchi jirani ya Kenya.


Hospitali hiyo ambayo itagharimu Sh7.9 bilioni hadi kukamilika kwake imewekwa jiwe hilo leo Jumatatu Julai 18, 2022.


Akitoa taarifa ya ujenzi wa hospitsli hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema kukamilika kwa Hospitali hiyo kutawezesha upatikanaji wa huduma bora za afya na itanufaisha wananchi 317,829 wa Wilaya hiyo.


"Kukamilika kwa Hospitali hii kutawezesha wananchi kupata huduma za kisasa na mpaka sasa hospitali imepokea vifaa tiba vyenye thamani ya Sh142.2 kati ya Sh 515.9 zilizotengwa kwa ajili ya manunuzi ya vifaa tiba vya hospitali hiyo pamoja na watumishi 30 wa Afya wakiwemo madaktari 5, wauguzi 15, mteknolojia wa vifaa tiba mmoja,"


Amesema awamu ya kwanza ya Hospitali hiyo itakamilika Septemba mosi mwaka huu na kwamba serikali imeshatoa Sh 3.49 Bilioni na fedha ambayo imeshatumika ni Sh 3.46 Bilioni ambapo yameshajengwa majengo 14 ambayo yamekamilika kwa asilimia 95, na katika mradi huo yatajengwa majengo 22.


Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Rombo wamesema Hospitali hiyo pia itachochea ukuaji wa maendeleo na uwekezaji katika ukanda wa chini wa Wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso