CHUO KIKUU AGA KHAN CHAWANOA WADAU JUU YA SAYANSI YA MALEZI,MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 6 July 2022

CHUO KIKUU AGA KHAN CHAWANOA WADAU JUU YA SAYANSI YA MALEZI,MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO



WADAU wa maendeleo ya awali ya mtoto nchiniTanzania,chini ya mradi wa 'Mtoto kwanza' unaotekelezw na mashirika ya CiC na TECDEN, wanapata mafunzo ya siku sitayanayowezeshwa na Chuo Kikuu cha Aga Khan,jijini Dodoma juu ya Sayansi ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto,ikiwa ni hatua ya kujenga ufanisi katika Programu Jumuishi ya kitaifa(JP-MMMAM, inayolenga kuhakikish watoto wote Tanzania wapo kwenye mwelekeo sahihi wa kufikia ukuaji timilifu.

NA MUTAYOBA  ARBOGAST, HUHESO DIGITAL DODOMA


Wadau hao ni waandishi wa habari vinara wa MMMAM,mmoja kila Klabu 26 za waandishi wa habari Tanzania bara na mbili kutoka Zanzibar,maafisa maendeleo ya jamii na maafisa ustawi wa jamii wa mikoa kumi ya Tanzania bara,kadhalika mashirika kumi yasiyo ya kiserikali(NGOs).


Akifungua mafunzo hayo,Waziri wa maendeleo ya jamii,wanawake na makundi maalum,amesema mafunxo hayo yana umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya mtoto na kuwa serikali iko tayari kuweka mifumo itakayohakikisha ufanisi wa PJ-MMMAM



Craig Ferla,mkurugenzi wa CiC Tanzania amesema kila mdau akitimiza wajibu wake ipasavyo,mradi huu utawafanya wazazi walezi na wote wanaohusjka na mtoto,kuwalea watoto katika misingi ifaayo katika makuzi yao,na hivyo kuwa watu wa kutumainiwa na taifa.


Victor Maleko,Afisa programu kutoka Muungano w a Klabu za habari nchini(UTPC),amesema katika kipindi cha miezi sita tu tangu Januari 2022,habari zaidi ya 400 zimeripotiwa na waandishi vinara,na kuwa wataendelea ba adhma hiyo ya kukusanya,kuchambua na kuchakata habari zinazowahusu watoto umri wa miaka 0 hadi nane.


Naye Joyce Marandu, Meneja raslimali watu wa Chuo kikuu Agha Khan,amesema wako tayari kuendeleza ushirikiano katika mradi na programu ya kitaifa,pindi wanapohitajika.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso