Michuano ya ligi ya IDDI
CUP katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga imezinduliwa
rasmi Jana kwa kuzikutanisha timu za Stand fc vs Chipukizi fc katika uwanja wa
Mnadani.
Mashindano hayo yanmefunguliwa
katika Kata ya Bulige kwenye Halmashauri hiyo na katika mchezo huo wa ufunguzi
Stand fc ilichapwa bao moja kwa nunge na timu ya Chipukizi fc na ligi hiyo
itachezwa katika Kata 18 za Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ikianza kwa ngazi ya vijiji hadi Kata.
Timu ya Chipukizi fc ikiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi mkuu wa kituo cha Polisi Busangi, Yusuph Chenge.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa mashindano hayo ambaye alikuwa ndio mgeni rasmi mkuu wa kituo cha
Polisi Busangi, Yusuph Chenge Adam alisema michezo hiyo itawapa fursa vijana ya
kujiendeleza kimichezo pia kuondokana na matukio ya kihalifu.
Michuano hiyo
imedhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Msalala, Iddi Kassim ambapo Bingwa wa
michuano hiyo atazawadiwa Ng’ombe mmoja, mshindi wa pili shilingi laki tano na
mshindi wa tatu shilingi laki tatu.
wananchi wakishuhudia mchezo wa Stand fc dhidi ya Chipukizi fc ikiibuka na ushindi wa bao 1-0
No comments:
Post a Comment