BASI LILILOKOSA MIKAPA YA ABIRIA LAKAMATWA LIKIWA NA WANAFUNZI 62 USIKU-IRINGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 30 July 2022

BASI LILILOKOSA MIKAPA YA ABIRIA LAKAMATWA LIKIWA NA WANAFUNZI 62 USIKU-IRINGA



Licha ya kutengenezwa baada ya kuharibika, Jeshi la Polisi, Kitengo cha Usalama Barabarani, Mkoani Iringa limezuia basi la Kimotco lililokuwa limebeba wanafunzi 62 na walimu saba wa Shule ya Msingi Camaldoli wilayani Mufindi lisiendelee na safari.


Jeshi hilo lilimelazimika kulizuia basi hilo baada ya kubaini halina mikanda ya abiria jambo ambalo ni hatari watoto.


Pia, basi hilo linadaiwa kuanza safari saa saba usiku kinyume cha sheria huku likiwa halijakaguliwa wala kupewa kibali cha kusafirisha wanafunzi.


Basi hilo limezuiwa wakati ikiwa zimepita siku chache baada ya wanafunzi 11 wanaosoma shule ya King David kupoteza maisha baada ya basi lao kutumbukia shimoni katika eneo la Mjimwema, Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkoani Mtwara.


Mkuu wa Kikosi cha Usalama, Barabarani Mkoani Iringa, Mosi Ndozero amesema ni kosa kisheria kwa basi lolote linalobeba wanafunzi kuanza safari usiku wa manane na bila kibali maalum cha kusafirisha abiria hao.


“Hii iwe ni onyo kwa mabasi mengine yote, ni marufuku kupakia wanafunzi bila kibali na kukaguliwa, lakini pia sheria hairuhusu safari za usiku.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso