Jeshi la polisi mkoa wa kagera limewataka madereva na watumiaji wa barabara kuwa makini na kufuata sheria za barabarani ili kuepukana ajali zinazogharimu uhai na maisha ya wananchi kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Jeshi la polisi ACP William .T. Mwampagale amesema ajali iliyotokea July 11 mwaka huu katika maeneo ya Busiri katika barabara kuu ya kutoka Lusahunga kuelekea Nyakahuru wilaya ya Biharamulo imesababisha vifo vya watu nane na watano wakiwa Ni familia moja.
Aidha amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili RAF 129W ikiwa ni treila lenye namba za usajili RL 4367 Aina ya Mercedes Benz lililokuwa likiendeshwa na Vicent Gakuba (52)mnyarwanda mkazi wa nyamata rugesela East province Rwanda kigari ambapo gari hiyo ilikuwa ikitokea rwanda kuelekea jijini Dar es salaam.
Pia ameongeza kuwa gari Hilo liligongana uso kwa uso na gali lenye namba T.626 DRX Aina ya Toyota succeed lililokuwa likiendeshwa na ndg. Nyawenda Bihela (35) muha mkiristo mkazi wa Kijiji Cha kikoma kata ya Lusahunga wilaya ya Biharamulo ambapo gali Hilo lilikuwa likitokea Nyamalagala wilaya ya Biharamulo kuelekea benako wilaya ya ngara .
Sambamba na hayo marehe waliyo fariki katika ajali hiyo ni Nyawenda Bihela (35) Dereva na mmiliki wa Toyota succeed, Jesca Leonard (45), Magreth Sekanabo (14) Adidas Sekanabo (12),Zabron Sekanabo (6), Vestina Sekanabo (8) hawa wote ikiwa Ni kutoka familia moja , Michael Charles (28), na Majaliwa Kanundo (32) ambao walikuwa wamefuatana na Dereva wa Gari Aina ya Toyota ambapo mpaka Sasa maiti zao zipo katika kituo Cha afya Cha Nyakanazi.
Mtuhumiwa Vicent Gakuba, Dereva wa Gari namba RAF 129W Mercedes Benz alijaribu kutoroka Mara baada ya ajali hiyo lakini Jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata tarehe 11 July mwaka huu majira ya saa 10:00 huko katima kizuizi Cha kahaza Rusumo akiwa ndani ya Lori linaloelekea Rwanda akiwa katika harakati za kukwepa kukamatwa na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani Mara baada ya taratibu kukamili za kiupelelezi.
Chanzo:Fullshangwe
No comments:
Post a Comment