Abiria 41 waliokuwa wakisafiri na basi la
Happy Nation wakitokea Dar es Salaam kuelekea Mwanza, wamenusurika katika ajali
baada ya basi lao kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Morogoro, ACP Ralph Meela, chanzo cha
ajali hiyo iliyotokea leo ni uzembe wa dereva wa basi aliyeacha njia yake na
kulifuata lori hilo.
Katika ajali hiyo, dereva wa basi hilo la Happy Nation amejeruhiwa na amepelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi huku abiria wengine wote wakiwa salama.
CHANZO:Azamnews
No comments:
Post a Comment