Watu wasipungua 42 wamekufa na wengine kiasi 100 wamelazwa hospitali katika jimbo la magharibi mwa India la Gujarat baada ya kunywa pombe yenye sumu yenye kiambata cha Methanol.
Mamlaka za jimbo hilo zimesema watu kadhaa walianza kuugua mapema wiki hii na kisha kupoteza maisha baada ya kunywa pombe hiyo inayotengenezwa kienyeji na kusambazwa kwenye vijiji kadhaa vya jimbo la Gujarat.
Waziri wa Mambo ya ndani wa jimbo hilo Harsh Sanghavi amesema uchunguzi umebaini wahanga hao walikunywa pombe yenye kiwango cha juu cha kemikali ya Methanol iliyosababisha vifo.
Jimbo la Gujarat ambako ni nyumbani kwa waziri mkuu wa India Narendra Modi ni moja ya maeneo yanayopiga marufuku uuzaji wa pombe kali nchini India lakini kwa muda mrefu vyombo vya usalama vinashindwa kutekeleza zuio hilo.
Chanzo:DW
No comments:
Post a Comment