NA MWANDISHI WETU
Meneja Programu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Bw. Remmy Lema akiambatana na mratibu wa kanda ya nyanda za juu kusini, Bw. Gabriel John pamoja na Afisa mkuu wa dawati la wanachama, Bi. Lisa Kagaruki wametembelea taasisi ya Jitambue Lembuka Tanzania (JLT) iliyopo wilayani Kyela, mkoani Mbeya.
Katika ziara hiyo meneja programu ameutambulisha Mtandao na kazi unazofanya katika uratibu na utetezi wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania.
JLT imeanzishwa mwaka 2008 ikijishughulisha na ujengeaji uwezo jamii katika maeneo ya afya, kilimo na elimu kwa makundi ya vijana, wanawake na wazee.
Taasisi imekuwa ikifanya ufuatiliaji (SAM) katika maswala ya kilimo katika wilaya ya Kyela na kata zake na kufanikiwa kuwawezesha wakulima kuuza zao la Kakao (Cocoa) kwa bei stahiki na yenye manufaa kwao, kufufua ghala linalowawezesha wakulima kuhifadhi mazao yao kwa usalama.
JLT imewezesha kuthaminiwa kwa wakulima na makampuni wanunuzi ambao walikuwa wakichelewesha malipo baada ya ununuzi wa zao hilo.
JLT Inakiri kukumbana na changamoto kadhaa ikiwemo uelewa mdogo kutoka kwa jamii na hata serikali juu ya kazi zao.
Rasilimali fedha pia inatajwa kuwa changamoto kubwa inayoizuia taasisi kufikia mahitaji ya jamii kwa kiasi kikubwa na hivyo kufanya wanufaika kuwa wachache kuliko inavyokusudiwa. Hili limesababisha taasisi imeweza kufikia kata 9 kati ya 33 zilizopo wilayani Kyela.
Baada ya mazungumzo, Mtandao umekabidhi baada ya nakala za machapisho ya Mtandao. Pia Mtandao ameikaribisha JLT kujiunga na Mtandao ili kuwa sehemu ya wanachama zaidi ya 200 waliosambaa nchi nzima bara na visiwani wakitekeleza shughuli za utetezi.
No comments:
Post a Comment