WENYE MAGARI YALIYOUA IRINGA WANASAKWA WATAKIWA KUJISALIMISHA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 14 June 2022

WENYE MAGARI YALIYOUA IRINGA WANASAKWA WATAKIWA KUJISALIMISHA


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Wilbroad Mutafungwa, amesema wanaendelea kumtafauta mmiliki wa basi ndogo aina ya Costa pamoja na mmiliki wa lori aina ya Scania yaliyosababisha ajali na kuua watu 20 katika eneo la changarawe mjini Mafinga mkoani Iringa.


Kamanda Mutafungwa amesema kwamba wanawatafuta wamiliki hao kwa ajili ya mahojiano pamoja na dereva wa Scania kwani dereva aliyekamatwa ni wa ile gari ndogo.


"Tunamatafuta dereva wa Scania na mmiliki wake, na tunamtafuta mmiliki wa hiyo Costa lazima ahojiwe kwamba ilikuwje akaruhusu gari lake likabeba abiria kwenda Mbeya wakati halina leseni ya usafirishaji wa abiria,"amesema Kamanda Mutafungwa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso