Na PAUL KAYANDA HUHESO BLOG
ILI kufanya Uchimbaji wenye tija,
kikundi cha Wanawake wa Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
(UMS) wamuomba waziri Dkt. Doto Bitko awape leseni ya Uchimbaji wa
Madini ya Dhahabu katika kijiji cha Nyamishiga Kata ya Lunguya.
Wamesema kuwa serikali imewakabidhi
Rush ambazo mpaka sasa wanazisimamia vyema na wanakusanya maduhuli
ya serikali na kuongeza kuwa iwapo watapata leseni watafanya vizuri zaidi.
Mwenyekiti wa kikundi hicho Levina
Onesmo aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili Ofisini
kwake huku akisisitiza ombi lao lifanyiwe kazi hara kwa kuwa RUSH ni ya muda
mfupi kwa mujibu wa taratibu za tume ya madini ukilinganisha kwa sasa wanawake
wamekuwa wajasili na wanahitaji kunufaika.
“Kwa kweli zamani kulikuwa na mfumo
dume ambapo wanaume pekee waliamini kuwa watafanyanya shughuli ya Madini bila
wanawake tunamshukuru Mungu nasisi kama wanawake tumeweza kuthubutu na kwa sasa
tunasimamia maeneo yenye mfumuko wa Madini ya Dhahabu,” alisema Levina
mwenyekiti wa kikundi.
Aliendelea kusema kuwa Wanaiomba
Wizara na tume ya Madini kuendelea kuwaamini wanawake kwenye sekta hiyo kwani
niwaaminifu huku akitolea mfano kuwa mwanawake ni nidereva mzuri ni nadra sana
kupata ajari mbaya wakati akiendesha gari barabarani anakuwa ni mwangalifu na
kwamba serikali itumie uaminifu huo kuwapa leseni.
Emmanuel Charles ni mmoja kati ya
viongozi kwenye eneo la mgodi amekili wanawake kuwa waaminifu hivyo ameunga
mkono serikali iwaamini na kendelea kuwapa fursa ya kusimamia maeneo yanayoibukia
kuwa na Madini ya Dhahabu.
“Kwa kweli mimi sina shaka na kundi
la wanawake kwenye suala la kazi, kiukweli kwa sasa wanawake kupitia vikundi
vyao wanachapa kazi siyo eneo la madini peke ake bali hata biashara zingine ni
wamama wachache wanaokwama katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali
zinazoingiza kipato,” alisema Charles Mchimbaji Nyamishiga.
No comments:
Post a Comment