Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Generali Marco Gaguti ametoa saa 48 kwa mkurugenzi wa kampuni inayosambaza viuatilifu vya korosho vyenye nembo ya makonde kujisalimisha Polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Mkuu huyo alisema kuwa mpaka sasa watu saba wameshakamatwa kutoka katika Wilaya za Newala na Tandahimba.
Alisema kuwa mmiliki huyo anapaswa ajisalimishe yeye mwenyewe ili hatua zingine za kisheria ziweze kufanywa kutoka na na pembejeo hizo kukamatwa zikiwa hazikidhi viwango.
No comments:
Post a Comment