WAISLAMU KUCHANJWA CHANJO YA PILI YA UVIKO-19 KABLA YA KWENDA HIJA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 25 June 2022

WAISLAMU KUCHANJWA CHANJO YA PILI YA UVIKO-19 KABLA YA KWENDA HIJA



Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema waliochanjwa chanjo ya Uviko-19 mwaka mmoja au miaka miwili iliyopita hawataruhusiwa kwenda hija hadi watakaporudia kuchanja chanjo hiyo.


Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Juni 24,2022 na Mkurugenzi wa Hija wa Bakwata, Haidary Kambwili, katika semina ya mahujaji inayofanyika ofisi za Makao Makuu ya Bakwata jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi ya wahusika kwenda nchini Saudi Arabia kuhiji.


Kwenda kuhiji katika mji Makka uliopo nchini Saudi Arabia kwa mwenye uwezo ni moja kati ya nguzo tano za uislamu.


Kambwili amesema miongoni mwa masharti wanayopaswa kuyafuata wanaotaka kwenda hija ni kuchanja saa 72 kabla ya kuanza safari.


Kambwili amesema utaratibu huo wameelekezwa na nchi ya Saud Arabia ikiwa ni mkakati endelevu wa nchi hiyo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19.

chanzo:Mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso