Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu nchini Tanzania (CWT), Deus Seif na Mwekahazina wa chama hicho, Abubakari Allawi, wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka yao vibaya kwa kuchepusha Sh 13.9milioni mali ya CWT.
Hukumu hiyo imesomwa jana usiku Juni 28, 2022 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi yao ya uhujumu uchumu namba 39/2021 ilipoitwa.
Akitoa Hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate amesema mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa hao na kila mmoja atatumikia kifungo cha miezi sita jela.
" Mbali na adhabu hii, mshtakiwa kwa kwanza(Seif) utakapomaliza kutumikia kifungo chako utatakiwa kuilipa fidia CWT ya Sh 7,590,000, kwa upande wa mshtakiwa wa pili (Allawi) wewe utakapomaliza kutumikia kifungo hicho utatakiwa kuilipa fidia CWT kiasi cha Sh6.2 milioni, haki ya kukata rufaa ipo wazi" amesema Hakimu Kabate.
No comments:
Post a Comment