NA MUTAYOBA ARBOGAST,BUKOBA
Vijana hao,ni sehemu ya vijana walio katika mtandao wa Kulinda amani katika nchi za maziwa makuu(Great Lakes Network for Dialogue and Peace) kutoka nchi za Rwanda,DRC,Tanzania na Uganda,ambapo vijana 200 wamewahi kukutana mjini Goma,DRC katika kinachoitwa 'Shule ya amani',na watakutana kila nchi moja kwa mwaka.
Mratibu wa mradi huu wa kudumisha amani,Jimmy Luhende kutoka shirika la ADLG la jijini Mwanz,Tanzania,amesema lengo la mradi huu wa miaka mitano,ni kuwajengea uwezo vijana wawe na moyo wa kujenga,kulinda na kudumisha amani,kwani nguvu za vijana zisipotumika vizuri,zinaweza kuhatarisha amani yenyewe,na akawataka vijana kutotumika vibaya nyakati za uchaguzi ambapo ndipo vijana hukimbiliwa zaidi.
Amesema pia kuna mikutano ya nchi mbilimbili kuzungumzia amani,fursa na vikwazo na kushirikishana namna ya kwenda mbele katika kuzifikia fursa za kiuchumi,ambazo ndi kigez muhimu katika kudumisha amani.
Kijana Nabaggala Resty wa Uganda amesema ni vizuri vijana wakashirikishwa katika vyombo vya maamuzi ili sauti za vijana zisikike.
Naye Kijana Alex Heneriko wa Mutukula,Tanzania akaiomba TAMISEMI kutumia mfumo uliokuwepo wa maafisa kushughulikia mikopo ya vijana badala ya mtu kuomba kwa njia ya mtandao,kwani baadhi ya maeneo mtandao ni hafifu mno.
Spika wa mji wa Mutukula,upande wa Uganda,Kabangira Fred,ameiomba Tanzania kupunguza idadi za vizuizi vya barabarani(roadblocks) kwani vinawachelewesha wafanyabiashara wa nchi yake katika kuzifikia fursa.
No comments:
Post a Comment